Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal, PSG zawania saini ya Osimhen

Victor Osimhen.jpeg Arsenal, PSG zawania saini ya Osimhen

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Arsenal na Paris Saint-Germain zimeripotiwa kuwa kwenye vita kali ya kuwania saini ya straika wa Napoli na Nigeria, Victor Osimhen, 25, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo watakumbana na upinzani wa kutosha kutoka kwa timu kubwa zinazoshiriki ligi ya Saudi Arabia.

Osimhen ambaye mkataba wake na Napoli unatarajiwa kumalizika mwaka 2026, amekuwa akihusishwa kujiunga na PSG pia ambayo inatafuta mbadala wa Kylian Mbappe aliyeondoka mwisho wa msimu huu akiwa anatarajiwa kutambulishwa kwenye kikosi cha Real Madrid muda wowote kuanzia sasa.

Napoli ilikataa kumuuza staa huyu katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi licha ya timu nyingi kuonyesha nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji huyo ambaye alionyesha kiwango cha juu kwenye michuano ya Afcon 2023.

Ndoto ya staa huyu siku moja ni kucheza England na Arsenal ambayo jana ilitangaza kuwaacha wachezaji 19 inataka kutumia mwanya huo kuhakikisha inamshawishi atue kwao.

Hata hivyo, Chelsea inatajwa kuwa na uhitaji mkubwa wa fundi huyu mwenye uwezo wa juu wa kupachika mabao.

Msimu huu amecheza mechi 32 za michuano yote na kufunga mabao 17 ukiwa unaonekana kutokuwa bora kwake tofauti na misimu mingine tangu ameanza kuwika kwenye soka la Ulaya.

KOCHA wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amekutana na Mkurugenzi wa michezo wa Crystal Palace, Dougie Freedman jijini London kwa ajili ya kuwezesha mchakato wa kuwasajili beki wa timu hiyo Marc Guehi, 23, kiungo Eberechi Eze, 25, wote kutoka England na winga raia wa Ufaransa Michael Olise, 22, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

KIUNGO wa Manchester City na Ubelgiji, Kevin de Bruyne, 33, anatarajiwa kupokea ofa kutoka timu mbalimbali za Marekani na Saudi Arabia kwa ajili ya kujiunga nazo katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

De Bruyne amekuwa akihusishwa kuondoka Man City tangu mwaka jana kwa kile kinachoelezwa kwamba anahitaji kupata changamoto mpya. Mkataba wa staa huyu unamalizika mwaka 2025.

CRISTIANO Ronaldo amezungumza na wachezaji wawili aliowahi kucheza nao timu moja hapo zamani, ambao ni Nacho Fernandez wa Real Madrid na Casemiro, 32, wa Man United ili kuwashawishi wajiunge na Al Nassr katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Mastaa hawa wanahitaji kuondoka kwenye timu zao kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine.

Tottenham inafikiria kuweka ofa mezani kwenda kwa Nottingham Forest kwa ajili ya kumpata winga wa timu hiyo na England Callum Hudson-Odoi, 23, kabla ya mwezi huu kumalizika.

Odoi alionyesha kiwango bora kwa msimu uliopita.Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.

Newcastle United inapambana kuhakikisha inakamilisha mchakato wa kumsajili beki wa kati wa Bournemouth na England, Lloyd Kelly, 25, kabla ya wiki hii kumalizika.

Kelly ambaye alikuwa mmoja kati ya wachezaji tegemeo kwa msimu uliopita, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.

FULHAM imetuma ofa kwenda Arsenal kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu hiyo na England Emile Smith Rowe katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.Rowe amekua hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha washika mitutu hao . Staa huyu mwenyewe ameonyesha nia ya kutaka kuondoka ili kulinda kipaji chake.

Los Angeles Galaxy imeshamtumia ofa kiungo wa Borussia Dortmund Marco Reus ambaye atakuwa mchezaji huru siku chache zijazo.

Reus alikuwa akisubiri kucheza fainali ya Ligi ya Mbingwa dhidi ya Real Madrid ambao ndio ulikuwa mchezo wake wa mwisho akiwa na timu hiyo akiwa na umri wa miaka 35.

Chanzo: Mwanaspoti