Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal, Liverpool, Man City ubingwa wa nani?

 132865598 Titlerace Arsenal, Liverpool, Man City ubingwa wa nani?

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Gumzo la sasa kwenye Ligi Kuu England ni mbio za kufukuzia ubingwa, nani atachukua kati ya Arsenal, Liverpool na Manchester City?

Msimamo unavyosoma kwa sasa, Arsenal ipo kileleni baada ya kukusanya pointi 64 katika mechi 28 ilizocheza. Imeshinda 20, sare nne na vichapo vinne, huku imefunga mabao 70 na kufungwa 24, hivyo ina +46 ya tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Namba mbili, ipo Liverpool yenye pointi kama za Arsenal, 64, lakini yenyewe imezidiwa tofauti ya mabao na The Gunners. Kwenye mechi 28 ilizocheza kikosi hicho cha Anfield kimeshinda 19, sare saba na vichapo viwili, imefunga mabao 65 na kufungwa 26 hivyo ina +39 ya mabao.

Mabingwa watetezi, Man City wapo kwenye nafasi ya tatu, pointi moja nyuma ya timu hizo mbili za juu, wenyewe wamekusanya pointi 63 kwenye mechi 28.

Imeshinda mechi 19, imetoka sare sita na vichapo vitatu, ikifunga mabao 63 na kufungwa 28, hivyo ina +35 ya tofauti ya mabao.

Kila timu imebakiza mechi 10. Je, kwa mbanano huo wa timu hizo tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ni timu gani itatoboa na kunyakua ubingwa wa msimu huu wa 2023-24? Cheki hapo hapo ratiba ya kila timu.

ARSENAL: Man City, Luton, Brighton, Aston Villa, Wolves, Tottenham, Bournemouth, Man United, Everton, Chelsea.

LIVERPOOL: Brighton, Sheffield Utd, Man United, Crystal Palace, Fulham, West Ham, Tottenham, Aston Villa, Wolves, Everton.

MAN CITY: Arsenal, Aston Villa, Crystal Palace, Luton, Tottenham, Nottingham Forest, Wolves, Fulham, West Ham, Brighton.

Chanzo: Mwanaspoti