Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal, Chelsea ni wao tu kwa Osimhen

Victor Osimhen.jpeg Victor Osimhen

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Napoli inataka ofa itakayofikia Euro 100 milioni kwa timu yoyote inayohitaji huduma ya straika wao Victor Osimhen katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Mabosi wa Napili wapo tayari kumuuza Osimhen ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2026, na tayari ishamweka katika rada zao straika wa Chelsea Romelu Lukaku kama mbadala wake.

Arsenal na Chelsea ni miongoni mwa timu zinazohusishwa kuwa na mpango wa kutaka kumsajili fundi huyu wa kimataifa wa Nigeria.

Staa huyu ni miongoni mwa washambuliaji waliokuwa wakiwindwa na timu nyingi barani Ulaya katika dirisha lililopita lakini ilishindikana baada ya Napoli kugoma kumuuza.

Kwa sasa wapo tayari kumuuza ingawa na Chelsea na Arsenal zinatajwa kuwa miongoni mwa timu zinazohitaji kumsajili.

Osimhen ambaye msimu uliopita alicheza mechi 32 za michuano yote na kufunga mabao 16.

Chanzo: Mwanaspoti