Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal, Barcelona zapimana ubavu kwa Martin Zubimendi

Mikel Arteta Arsenal Transfer Martin Zubimendi Real Sociedad.png Martin Zubimendi

Tue, 14 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Barcelona inakumbana na upinzani mkali kutoka kwa Arsenal na Juventus katika harakati za kuwania saini ya kiungo wa Real Sociedad, Martin Zubimendi dirisha lijalo la kiangazi.

Kwa mujibu wa Mundo Derpotivo, Barca imekuwa ikituma wawakilishi kumtazama Zubimendi katika mechi anazocheza msimu huu na kiwango chake pamoja na staili yake ya uchezaji.

Mbali ya wababe hao kutoka Nou Camp, Arsenal pia inataka kumsajili kiungo huyo ili kuziba pengo la Thomas Partey ambaye kocha Mikel Arteta amekubali auzwe kwa sababu muda mwingi amekuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha ya mara kwa mara hali inayosababisha kuwa na mchango mdogo kwenye timu.

Zubimendi anaonekana kuwa mtu sahihi wa kuziba pengo la Partey kwa sababu staili yake ya uchezaji inaendana na vile ambavyo Arteta anataka. Tangu kuanza kwa msimu huu kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania amecheza mechi 45.

KIUNGO wa Al-Ettifaq ya Saudi Arabia anayecheza kwa mkopo Ajax, Jordan Henderson huenda akarudi Saudia Arabia au akajiunga na timu nyingine barani Ulaya baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya. Henderson mwenye umri wa miaka 33, bado ana mkataba na Ettifaq hadi 2026. Akiwa na Ajax msimu huu mchezaji huyo amecheza mechi 29 za michuano yote.

PARIS St-Germain imejiondoa katika mpango wa kutaka kumsajili kiungo wa Newcastle United na Brazil, Bruno Guimaraes katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kutokana na kiasi kikubwa cha pesa ambacho Newcastle inakitaka ili kumuuza staa huyo ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa 2026. Kwa mujibu wa ripoti Newcastle inahitaji dau lisilopungua Pauni 100 milioni ili kumuuza Guimaraes.

MBALI YA St Louis City iliyotajwa tangu awali, sasa Inter Miami na Al-Nassr zimeripotiwa kuanza mazungumzo na mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani, Marco Reus ili kumsajili dirisha lijalo. Reus mwenye umri wa miaka 34, anaondoka Dortmund dirisha lijalo la kiangazi na vigogo wengi wameonyesha nia ya kutaka kumsajili. Msimu huu amecheza mechi 39 za michuano yote.

MABOSI wa Juventus wanaangalia uwezekano wa kusajili straika dirisha lijalo la majira ya kiangazi na hadi sasa wamewaweka katika rada mshambuliaji wa Manchester United, Mason Greenwood anayecheza kwa mkopo Getafe na straika wa Bologna na Uholanzi, Joshua Zirkzee, 22 (pichani). Mastaa hawa wameonyesha viwango bora msimu huu.

AC Milan imeanza mazungumzo na Fiorentina kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu hiyo na Morocco anayecheza kwa mkopo Manchester United, Sofyan Amrabat katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Man United inadaiwa haina mpango wa kumsainisha mkataba wa kudumu Amrabat mwenye umri wa miaka 27 ambaye msimu huu amecheza mechi 26 za michuano yote.

BEKI wa Arsenal na Scotland, Kieran Tierney, 26, anadaiwa kutamani kuondoka mazima mikononi mwa washika mitutu hao katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Tierney mwenye umri wa miaka 26, msimu huu anacheza kwa mkopo Real Sociedad na amepanga kusaini mkataba wa kudumu na timu hiyo na ikishindikana atimkie sehemu nyingine.

TOTTENHAM Hotspur ipo katika hatua nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Brentford na England, Ivan Toney, ambaye imemuandalia ofa ya Pauni 50 milioni ili kuhakikisha inampata katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Toney mwenye umri wa miaka 28, amekuwa akiwindwa na vigogo wengi u kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu.

Chanzo: Mwanaspoti