Michuano ya kombe la Mataifa ya Amerika ya Kusini Copa America 2024 imeanza kutimua vumbi usiku wa kuamkia leo ambapo Mabingwa watetezi, Argentina wamefungua michuano kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Canada kwenye uwanja wa Mercedes-Benz huko Atlanta, Georgia Marekani.
Kiungo wa Liverpool, Alexis Mac Allister alitoa pasi ya bao la kwanza lililofungwa na Julian Alvarez wa Man City huku nahodha Lionel Messi akitoa pasi saidizi ya goli la pili lililofungwa na Lautaro Martinez wa Inter Milan.
Mabao ya Argentina katika mchezo huo uliohudhuriwa na idadi kubwa ya mashabiki yamefungwa na Alvarez 49’, Martinez 88’.
NB: Copa America ndio mashindano kongwe zaidi ya soka ya mabara Duniani kwa wanaume yanayoshindaniwa na timu za taifa kutoka Amerika Kusini.
Mashindano hayo huamua bingwa wa Amerika Kusini ingawa kuanzia miaka ya 1990, timu kutoka Asia na Amerika Kaskazini pia zimekuwa zikialikwa kushiriki. Wenyeji wa Copa America 2024 ni Marekani.