Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Argentina timu ya kwanza kuifunga Brazil nyumbani

Messi Args.jpeg Argentina timu ya kwanza kuifunga Brazil nyumbani

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Brazil imepoteza mchezo wa nyumbani wa kufuzu kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kihistoria kufuatia kipigo cha 1-0 dhidi ya Mabingwa wa Dunia Argentina katika dimba la Maracanä mjini Rio de Janeiro.

FT: Brazil 0-1 Argentina

⚽ Otamendi 63’

???? Joelinton 81’

Brazil imepoteza mechi mbili tu za nyumbani kwa kipindi cha miaka 70 na mara zote dhidi ya Argentina, dhidi ya Lionel Messi.

Brazil inapitia wakati mbaya kwa sasa baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2001 na huenda wakafikia rekodi ya miaka 22 iliyopita ya kupoteza mechi nne mfululizo ikiwa watapoteza dhidi ya England katika dimba la Wembley mwezi Machi 2024 kabla ya kuivaa Uhispania katika dimba la Santiago Bernabeu.

Mechi hiyo ilichelewa kwa takribani nusu saa baada ya kutokea mzozo mbaya kati ya mashabiki wa timu hizo kupigana kwenye Uwanja wa Maracana mjini Rio de Janeiro, Brazil.

Baada ya kuona hali hiyo, mshindi wa Ballon d ‘Or 2023, Lionel Messi alikimbia hadi eneo la tukio katika juhudi za kutuliza hali hiyo kabla ya kuwaongoza wachezaji wenzake wa timu ya Argentina kutoka uwanjani kuandamana kilichotokea.

Wachezaji walikaa kwenye chumba cha kubadilishia nguo hata baada ya muda uliopangwa wa mechi kuanza kufikika.

Washindi hao wa kombe la dunia walirejea baada ya dakika 22 kwenye chumba cha kubadilishia nguo, na wakafanya mazoezi kwa dakika kadhaa kabla ya mchezo huo kuanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live