Timu ya taifa ya Argentina hivi sasa ipo mbioni kuelekea kuivunja rekodi ya dunia ya kuwa miongoni mwa taifa ambalo halijapoteza mchezo wowote kimataifa kwa miaka 3 mfululizo, ambapo hivi sasa rekodi hiyo inashikiliwa na na timu ya taifa ya Italia.
Italia wanashikilia rekodi hiyo kwa kucheza jumla ya mechi 37 bila kupoteza tangu mwaka 2018 mpaka mwaka 2021 walipopoteza mchezo wao kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Hispania katika michuano ya UEFA kwa ngazi ya timu ya taifa.
Argentina wanaikimbilia kuvunja rekodi hio wakiwa wamecheza michezo 35 bila kupoteza kwa miaka mitatu mfululizo tangu Julai 6 mwaka 2019 walipocheza dhidi ya Chile katika michuano ya Copa America na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, mpaka hii leo 2022 hawajapoteza mchezo wowote.