Mon, 1 Jan 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Chama cha Soka cha Argentina (AFA) kimepanga kustaafisha 'jezi' namba 10 ya Lionel Messi ambayo awali ilikuwa ikivaliwa na Diego Maradona.
Mipango ya kuistaafisha 'jezi' hiyo ni kuheshimu mchango wa Messi katika timu hiyo baada ya kushinda Kombe la Dunia la 2022, taji la kwanza kwa taifa hilo tangu 1986, pamoja na 2021 Copa America.
Rais wa chama hicho Claudio Tapia, mbele ya waandishi wa habari amesema Messi atakapostaafu kuitumikia timu ya taifa, hatoruhusiwa mtu mwingine yeyote kuvaa 'jezi' nambari 10 badala yake itakuwa imestaafishwa kwa ajili ya kuweka heshima kwa mchezaji huyo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live