Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Argentina amepata ubingwa kwa Jasho na Damu, mashabiki tumepewa burudani tosha

Mbappe Messi Mkl.jpeg Argentina amepata ubingwa kwa Jasho na Damu, mashabiki tumepewa burudani tosha

Mon, 19 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbungi limepigwa likapigika. Fainali ya mwaka huu imekua bora sana. Hadi dakika ya 80 France walikua nyuma kwa bao 2. Kila mtu alijua kazi imekwisha.

Wenye roho nyepesi walishaanza kuondoka uwanjani. Lakini meza ilivyopinduliwa kibabe na bwana mdogo kutoka Tarakea, Kylian Mbappé "Tarimo" ni hadithi isiyotarajiwa. Dakika 120 za nyongeza ilikua kama kutizama movie ya Jackie Chan.

Argentina amepata ubingwa kwa jasho na damu. France nao wamejaribu kutetea ubingwa wao kwa jasho na damu. Mashabiki tumepewa burudani ambayo tuliikosa miaka mingi.

Argentina wametufundisha kukaza hata unapokua kwenye kilele cha mafanikio, usibweteke. Hakuna kitu kinakuja kirahisi. France nao wametufundisha usikate tamaa hata kama unaona muda umekwisha.

Pigana kiume. Kaza. Sekunde chache zinaweza kufanya maajabu na kubadili historia ya maisha yako. Hongera Buenos Aires, hongera Paris. Fainali ya kihistoria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live