Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arajiga yamemnyookea sasa kazi kwake

Arajiga Awafuata Ahmed Arajiga

Thu, 16 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Huu unaweza kuwa msimu mzuri wa soka kwa refa wa Tanzania mwenye beji ya Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), Ahmed Arajiga kutokana na uzito wa michezo aliyochezesha.

Ni nadra kuona refa mmoja wa kati akichezesha mechi ya watani wa jadi, Yanga na Simba katika msimu mmoja lakini kwa Arajiga imekuwa tofauti na alichezesha mechi ya mzunguko wa kwanza na kisha ya ule wa pili kwenye ligi msimu huu.

Baadaye akapata fursa ya kuchezesha mechi za soka za michezo ya Afrika (All African Games) iliyofanyika Ghana kuanzia Machi 8 hadi Machi 23 mwaka huu.

Ukiondoa hilo, akapata pia fursa ya kuchezesha mechi iliyokuwa na mvuto na msisimko mkubwa ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu baina ya Azam na Simba hivi karibuni.

Kabla hata hajapoa baada ya kuchezesha mechi ya Azam na Simba, Arajiga mwanzoni mwa wiki hii amepata uteuzi na Fifa wa kuchezesha mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia kati ya Malawi na Sao Tome&Principe, Juni 6 mwaka huu jijini Lilongwe kwenye Uwanja wa Bingu.

Katika uteuzi huo, Arajiga ameteuliwa kuwa mwamuzi wa kati na atasaidiwa na Frank Komba na Kassim Mpanga huku mwamuzi wa akiba akipangwa kuwa Hery Sasii wote wakiwa wanatoka Tanzania.

Kuna kila sababu ya kumpongeza Arajiga kwa hiki ambacho anakifanya kwani amekuwa akizitendea haki mechi hizo alizopata nafasi ya kuchezesha jambo ambalo linashawishi mamlaka ziendelee kuwa na imani kubwa kwake.

Hata hivyo, mafanikio ambayo Arajiga anapata hivi sasa ni deni kwake la kutakiwa kufanya vizuri katika michezo ambayo atapangwa kuchezesha siku za usoni ili sifa anazopata ziwe na mwendelezo.

Hatakiwi kujiona kama ameshamaliza na kuanza mambo yasiyofaa ambayo yanaweza kumharibia mazuri yote ambayo ameyafanya na kumwondoa kwenye uwezekano wa kutimiza ndoto zake nyingi ambazo anaziota kupitia urefa.

Chanzo: Mwanaspoti