Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arafati Haji: Hatutabadili kanuni tuliyowapiga Simba tano

Arafat Ahimiza Mashabiki Yanga, Simba Kushirikiana Kimataifa Arafati Haji.

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Klabu ya yanga, Arafati Haji amesema kuwa hawana mpango wa kubadili mbinu yao ya ushindi walioitumia wakati wa mchezo wao wa Novemba 5, 2023 dhidi ya watani zao Simba, kuelekea mchezo wa dabi ya Kariakoo Aprili 20, 2024.

Haji amesema kuwa hawana sababu ya kuondoka Avic Town Kigamboni na kwenda sehemu nyingine kuweka kambi kwani kambi yao imekuwa ikiwapa matokeo chanya tangu wameanza kuitumia misimu kadhaa sasa.

“Tumejiandaa kikamilifu na tutaingia kwenye mchezo wa dabi kivingine tukiwa tumefuta matokeo yote ya nyuma yaliyotokea kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba. Huu ni mchezo mpya lazima ujipange kulinaga na mchezo husika.

“Sisi hatuwezi kutoka nje ya kambi yetu kwa sababu pale Avic Town ndiyo kambi bora kuliko kambi yoyote kwenye ukanda wetu huu, kuna utulivu wa kutosha na concentration ya mechi iko juu. Mechi tuliyowapiga bao tano tulitokea Avic Town kwa hiyo huwezi kubadilisha kanuni yako ya ushindi (winng formula).

“Dabi ni dabi huwezi kuifananisha na mechi nyingine, ina mambo mengi na tutaiendea kitofauti, tumewapa wazee na wazee wameipokea vizuri,” amesema Arafati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: