Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arafat Haji anataka trending - Oscar Oscar

Arafat Haji A Ah Arafat Haji

Mon, 4 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga kwa sasa imekuwa ya timu ya trending,wanafanya mambo ama kuzungumza vitu ambayo kiuhalisia bado hawana uwezo na ndio kwanza wanajitafuta huku Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Kabla ya mchezo vs Al Ahly,Ofisa Habari wa Yanga Ally Shaabani Kamwe alisema kuwa watawaonyesha Man City jinsi ya kumfunga Al Ahly ila kilichotokea jana mmekiona maana kila kitu Yanga wamezidiwa.

Juzi baada ya mchezo kumalizika Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji, amesema kwamba kuna mtu wa Al Ahly amemwambia kwamba watacheza fainali ya CAFCL vs Al Ahly. Hivi Arafat unaijua fainali wewe? Unadhani huku kuna wakina Marumo Gallants?

Yanga eehh hebu jipangeni na michezo iliyosalia,Yanga hamna uwezo huo wa kucheza fainali ya CAFCL labda itokee bahati tu kama ile ya Leicester City walivyoshinda EPL msimu wa 2015/2016.

Si mnawaona hao Wydad Casablanca waliocheza fainali msimu uliopita ila wameanza kwa kuchechemea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live