Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arafat Haji: Yanga bado hatujamaliza usajili

Ricardo 75569 icardo Emmanuel Mahop.

Mon, 24 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Yanga SC, Arafat Haji amesema kuwa bado wanaendelea na maboresho ya kikosi hicho hivyo wanaendelea na usajili katika maeneo ambayo wanaona kuwa yanahitaji kuboreshwa.

Arafat amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa tamasha la SIku ya Mwananchi juzi huku mashabiki wakiwa njiapanda kuhusu kutokuwepo kwa baadhi ya nyota wa kikosi hicho kama Yanick Bangala, Djuma Shabani, Mamadou Doumbia na Fiston Mayele.

"Wananchi hongereni sana mmependezesha na kunogesha Kilele cha wiki ya Mwananchi kwa hakika tukio letu limefana na kufanikiwa kwa 100%.

"Wachezaji wenu wapya mmewaona na mmeona uwezo wao kupitia mechi ya kirafiki dhidi ya timu kubwa na yenye heshima Afrika kusini na Afrika kwa ujumla"

"Tunaendelea kuboresha kikosi chetu kwa ajili ya kutetea mataji yetu tukiyoshinda ndani ya nchi lakini pia kuhakikisha tunafanya vizuri kimataifa kama ilivyokuwa msimu uliopita," amesema Arafat Haji.

Taarifa kutpoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa, baada ya kumuuza Mayele kwenda Pyramids FC ya Misri, Yanga tayari wameshamalizana na straika mpya Ricardo Emmanuel Mahop raia wa Cameroon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: