Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arafat Haji: Safari moja ya Yanga Tsh milioni 230

Yanga Dar Es Salaam Arafat Haji: Safari moja ya Yanga Tsh milioni 230

Thu, 25 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Klabu ya Yanga, Arafat Haji amedai kuwa ni gharama kubwa kuendesha klabu kwani pesa za matumizi zinazotakiwa kuwatunza wachezaji na kuwasafirisha kila mchezo ni kubwa hivyo vilabu vingi vidogo vinashindwa kumudu.

"Dola 100,000 (zaidi ya Sh230 milioni) kwa safari moja ni gharama kubwa sana na sio chini ya michezo mitatu kwenda kucheza bado pia changamoto ya safiri ndani ya Afrika tuna ndege chache za kwenda moja kwa moja kwenda baadhi ya nchi.

"Tunatumia saa 18 kusafiri mahitaji makubwa yanahitajika kuhifadhi timu kupumzika sehemu nzuri, chakula kizuri hivyo gharama ni kubwa, ni timu chache Tanzania zinaweza kumudu hivyo tunaomba bajeti kwa upande wa Serikali ili timu ziweze kushiriki vizuri.

"Yanga tayari imekuwa chapa kubwa ya kuitangaza Tanzania hivyo mpira ukipewa kipaumbele ni biashara kubwa mfano usajili wa wachezaji wa kigeni lazima walipiwe vibali vya kuishi na kufanya kazi pesa inaingia Serikalini,” Arafat Haji Makamu wa Rais wa klabu ya Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: