Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arafat Haji: Mafanikio ya Yanga ni mafanikio ya Tanzania nzima

Arafat Pic Data Makamu wa Rais Yanga, Arafat Haji

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga ilipitia kipindi kigumu sana mwaka 2018-2019, nafikiri lile lilikuwa ni fundisho kubwa ambalo limetusaidia kujipanga upya na mafanikio ambayo tumetapata hayajatokea kwa bahati mbaya.

Ni matunda ya mipango na mikakati ambayo tulijiwekea katika kuhakikisha tunaivusha timu na kuifikisha mbali, kwetu ni furaha na faraja kubwa kuona timu yetu imetoa wachezaji wengi wanaowania tuzo za CAF kwa mashindano ya msimu uliopita.

Mafanikio ya Yanga ni mafanikio ya Tanzania, ndio maana Yanga inatoa wachezaji wengi kwenye timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kwa hiyo huwezi kuitengenisha Yanga na mafanikio ya timu ya Taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live