Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arafat Haji: Gamondi yupo sana Yanga, Wapinzani watateseka mno

Hersi X Gamondi CRDB Kocha gamondi na Eng. Hersi.

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Klabu ya Yanga, Arafat Haji amesema kuwa Kocha Mkuu wa Timu hiyo, Angel Miguel Gamondi ataendelea kusalia katika Mitaa ya Twiga na Jangwani msimu ujao licha ya kumaliza mkataba wake wa sasa.

Arafat amesema kuwa tayari mazungumzo yako mwishoni kukamilisha taratibu za Muragentina huyo kusaini mkataba mpya, hivyo mashabiki wa timu hiyo wasiwe na hofu kwani mwalimu huyo aliyewapa mafanikio makubwa msimu huu ataendelea kusalia kwenye kikosi hicho.

kauli hiyo ya haji inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Gamondi kusema kuwa hana uhakika iwapo msimu ujao atasalia Yanga kwani amemaliza mkataba wake wa mwaka mmoja na hajasaini mkataba mpya huku akiwaaga mashabiki wa timu hiyo akielekea nyumbani kwao kwa ajili ya mapumziko.

“Ni kweli mkataba wake ulikuwa wa msimu mmoja lakini ataendelea kubaki Yanga. Tumeshaanza siku nyingi taratibu za kumbakisha lakini tulikuwa tunasubiri kwanza kumaliza msimu ili tuweze kuwa na utulivu wa kumalizia palipobakia.

“Kwa kweli sisi Wananchi tumeridhika na alichotufanyia Miguel Angel Gamondi, amekidhi haja ya Wananchi na Klabu yetu, na soka zuri kabisa, ameweka rekodi ya alama 80, rekodi ya mabao mengi kabisa kwa msimu mmoja, ni mwalimu ambaye anakidhi.

“Rais wetu alisema kwamba hili kombe tutalichukua miaka mingine mitano ijayo, vilevile tutakuwa na Gamondi kwa miaka mingi, kwa hiyo miaka mingine mitano ijayo Wananchi wataendelea kula bata katika soka. Sisi tumejipanga kuwa machampioni wa kihitosria Tanzania,” amesema Arafat Haji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live