Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arafat Haji: Dabi itumike kuboresha viwanja visifungiwe

Arafat Pic Data Klabu ya Yanga, Arafat Haji.

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Klabu ya Yanga, Arafat Haji amesema anatamani kuona dabi inatumika kuboresha viwanja kutokana na mapato yanayopatikana mlangoni.

“Baadhi ya viwanja pia vinavyotumika kuchezewa mechi za Ligi Kuu vimekuwa vikifungiwa kutokana na kutokuwa na ubora. Hii ni kutokana na kukosa fedha za kuboresha viwanja.

“Mfano tukitenga bajeti ya mapato ya viwanjani kwa ajili ya kuboresha viwanja tutapata timu ya taifa imara, kutokana na viwanja vingi vitakavyoboreshwa kutumiwa na vijana ambao sasa wanacheza katika mazingira magumu.”

Haji amebainisha hayo, Novemba Mosi 2023 wakati akichangia mada kwenye mjadala wa Mwananchi Space, mada isemayo Simba, Yanga zitumiaje dabi ya Karikoo kibiashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live