Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Apigwa Faini kwa kujisaidia Uwanjani

Ajisaidia Uwanjani Apigwa Faini kwa kujisaidia Uwanjani

Wed, 22 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka za soka nchini Nigeria zimeilipisha faini ya takribani dola za Kimarekani 1,000 klabu ya daraja la kwanza huko Ibadan baada ya afisa wao kujisaidia uwanjani.

Picha iliyomuonyesha afisa huyo akijisaidia haja ndogo kabla ya kuanza kwa mechi kati ya Shooting Stars na Akwa United Jumapili iliyopita ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuleta fedheha.

Afisa huyo Auwal Mohammed pia amesimamishwa kwa mwaka mmoja na hatoruhusiwa kujihusisha na shughuli zozote zinazohusiana na Ligi ya soka ya nchini Nigeria (NPFL).

Uongozi wa NPFL umekielezea kitendo hiko kilichofanyika wazi huku kikishuhudiwa na umma kuwa ni cha dharau na ambacho kimeiletea soka sifa mbaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live