Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anwar Mbinde: CV ya Gamondi tuione Uwanjani

Anwar Mbindeee Anwar Mbinde: CV ya Gamondi tuione Uwanjani

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Klabu ya Yanga kumtangaza Miguel Angel Gamondi kuwa Kocha Mkuu wa Timu hiyo akimrithi Nasreddine Nabi alieachana na Timu hiyo.

Wasifu wa Muargentina huyo unaonesha amepita katika Vilabu mbalimbali vikubwa Barani Afrika huku akiwa na uzoefu usiopungua miaka 20 katika soka la Afrika.

Sasa ukubwa wa Cv (Wasifu) wa Kocha huyo Mchambuzi wa Michezo kutoka Wasafi FM, Anwar Mbinde anasema CV ya Gamondi ni jambo moja na ubora wa uwanjani ni jambo jingine.

Akizungumza Anwar anasema;

"Gamondi watu wote tushafahamu kuwa ni Kocha wa namna gani, kwa Vilabu tu alivyopitia tunaona ni kwa namna gani analifahamu Soka la Afrika"

"Lakini tu cha msingi niwaambie Wanayanga, Viongozi na wadau wote wa mpira nchini kuwa kwa sasa waache kututishia na CV ya Kocha cha msingi tuuone ubora huo Uwanjani, ni namna gani atatengeneza kikosi kitakachowasahaulisha Mashabiki Kocha alieondoka"

Je una matumaini gani na Kocha mpya wa Yanga? ataziba pengo la Nasreddine Nabi? Tuachie maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: