Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Antony atambulishwa ndani ya uzi wa Man United

A 2223 Hero Article Copy 31661979127072 Medium Anthony

Thu, 1 Sep 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Nyota mpya wa Manchester United, Antony, 22, ametambulishwa rasmi baada ya kukamilisha uhamisho wake uligharimu kitita cha Pauni 85.5 milioni.

Man United ilikubali kutoa mkwanja huo baada ya mazungumzo ya muda mrefu kwani Ajax iligoma kumuuza winga huyo.

Winga huyo wa Kimataifa Brazil anaamini Erik ten Hag atamsaidia kiwango chake kuimarika zaidi kwani wanafahamiana kwa muda mrefu.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano kukipiga Old Trafford, Antony amesema ana furaha kujiunga na Man United moja ya klabu kubwa duniani.

"Nawashukuru mashabiki zangu kwa kuniamini, kucheza chini ya Ten Hag jambo jema kwa upande wangu, kocha mzuri kutokana na mbinu zake za kiufundishaji, ameniambia kuhusu mipango yake nina shauku kubwa ya kucheza kufikia malengo ya kocha,” alisema Antony.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz