Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Antony agoma kuondoka Manchester United

Antony Man Utd Antony agoma kuondoka Manchester United

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Winga wa Manchester United na Mbrazil, Antony, 24, ambaye hivi karibuni iliripotiwa yupo kwenye mipango ya kupigwa bei na mabosi wa mashetani hao wekundu, amekataa kuondoka na kuwaambia anahitaji kupambania nafasi katika kikosi cha kwanza.

Ripoti za awali zilieleza Man United ipo kwenye mazungumzo na Fenerbahce ili kumuuza huko ikiwa ni sehemu ya kupunguza matumizi.

Staa huyu wa kimataifa wa Brazil ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwa pesa nyingi zaidi katika kikosi cha Man United.

Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi moja tu kwenye muendelezo wa Ligi Kuu England na aliingia akitokea benchi akicheza dakika moja.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 lakini kuna kipengele cha Man United kuurefusha kwa msimu mmoja zaidi.

Kieran Trippier

TIMU za Uturuki, Istanbul Basaksehir, Fenerbahce, Besiktas na Eyupspor zimekata tamaa kwenye mipango yao ya kutaka kumsajili ya beki wa Newcastle United, Kieran Trippier baada ya mabosi wa timu yake kusisitiza hawataki kumuuza au kumtoa kwa mkopo kwa sasa. Trippier mwenye umri wa miaka 33, ilidaiwa anataka kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha.

Jhon Duran

INAELEZWA timu mbalimbali ziliwasilisha ofa zinazofikia 40 kwa ajili ya kumsajili straika wa Aston Villa, Jhon Duran dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini Villa ilikataa zote. Licha ya kushindwa kumpata wakati huo, taarifa kutoka tovuti ya The Mirror zinaeleza timu hizo zinataka kuwasilisha tena ofa mwakani dirisha la majira ya baridi na kiangazi.

Juanlu Sanchez

MANCHESTER United inafuatilia kwa karibu maendeleo ya beki wa kulia wa Sevilla, Juanlu Sanchez, 21, na inaweza kuwasilisha ofa kwa ajili ya kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya baridi. Mabosi wa Man United bado wanahitaji kuweka sawa eneo lao la ulinzi ambalo licha ya usajili uliofanywa dirisha lililopita la majira ya kiangazi bado linaonekana kuwa na mapungufu.

Marc Guehi

KOCHA wa Newcastle, Eddie Howe na Mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo, Paul Mitchell wamemaliza tofauti zao na nguvu zao sasa wamezielekezea kwenye usajili wa dirisha lijalo la majira ya baridi na mchezaji wa kwanza waliyepanga kumsajili ni beki wa Crystal Palace na England, Marc Guehi, 24, ambaye walishindwa kufanikisha mchakato wa kumsajili dirisha lilopita la majira ya kiangazi.

Liam Cooper

BEKI wa zamani wa Leeds United na Scotland, Liam Cooper, 33, yupo katika hatua za mwisho kujiunga na CSKA Sofia ya Bulgaria kwa usajili huru. Cooper ambaye kwa sasa ni mchezaji huru tangu aachane na Leeds katika dirisha lililopita la majita ya kiangazi. Akiwa na timu hiyo alicheza mechi 19 za michuano yote.

Cristian Romero

TOTTENHAM imesisitiza haina mpango wa kumuuza beki wao raia wa Argentina, Cristian Romero, 26, licha ya timu mbalimbali zikiwamo Manchester United, Real Madrid na Paris St-Germain kuonyesha nia ya kumsajili. Timu hizo nyingi zilijaribu kumsajili Romero dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana lakini ilishindikana na bado zinaangalia uwezekano wa kumsajili dirisha la majira ya baridi mwakani.

Carney Chukwuemeka

GALATASARAY imeonyesha nia ya kutaka kumsajili winga wa Chelsea, Carney Chukwuemeka, 20, dirisha hili kwa mkopo wa msimu mmoja. Chukwuemeka ni mmoja wa mastaa ambao kocha wa Enzo Maresca amewaambia watafute timu za kucheza msimu huu kwani hawapo katika mipango yake.

Chanzo: Mwanaspoti