Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Antony, Rashford pasua kichwaa Manchester United

Rashford X Anthony Antony, Rashford pasua kichwaa Manchester United

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag amegoma kuwafuta mastaa wake Antony na Marcus Rashford kwenye mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Liverpool utakaofanyika huko Marekani usiku wa kuamkia kesho Jumapili.

Mawinga hao waliumia kwenye mechi ya ushindi ya mabao 3-2 dhidi ya Real Betis katikati ya wiki iliyopita, ambapo Rashford alianza kwenye kikosi cha kwanza na kufunga bao la kwanza la Man United kwa mkwaju wa penalti.

Hata hivyo, Mwingereza huyo hakumaliza mechi hiyo baada ya kuumizwa na kiungo wa Betis, Sergi Altimira kwenye enka na kulazimika kutoka uwanjani. Kutolewa na Rashford kulikuja muda mfupi baada ya Antony kuingia kuchukua nafasi ya Amad Diallo, lakini Mbrazili huyo naye hakumalizia dakika 90 za mchezo huo.

Man United imeonekana kupata pigo kwenye ziara yao hiyo ya Marekani baada ya beki wao mpya, Leny Yoro kuumia mfupa wa mguu na kumfanya awe nje kwa miezi mitatu alipoumia kwenye mechi dhidi ya Arsenal, wakati straika Rasmus Hojlund naye atakuwa nje kwa wiki sita kutokana na kupata maumivu ya misuli ya paja.

Hata hivyo, kocha Ten Hag anaamini Antony na Rashford watatumika kwenye mchezo huo dhidi ya Liverpool utakaofanyika kwenye Uwanja wa Williams-Brice, huko Carolina. Lakini, pia kocha huyo Mdachi, anaweza kuchagua kutowatumia ili kuwaweka fiti kwa ajili ya mechi ya wikiendi ijayo ya Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wa mji mmoja, Manchester City. Na kama Antony na Rashford watashindwa kucheza wikiendi hii, basi Mason Mount na Hannibal Mejbri wanaweza kupata nafasi ya kucheza kwa kuwa Alejandro Garnacho bado yupo mapumzikoni tangu aliposhinda ubingwa wa Copa America akiwa na Argentina.

MECHI 10 ZA KWANZA ZA LIGI MAN UTD

-Agosti 16 vs Fulham (nyumbani)

-Agosti 24 vs Brighton (ugenini)

-Agosti 31 vs Liverpool (nyumbani)

-Septemba 14 vs Southampton (ugenini)

-Septemba 21 vs Crystal Palace (ugenini)

-Septemba 28 vs Tottenham (nyumbani)

-Oktoba 5 vs Aston Villa (ugenini)

-Oktoba 19 vs Brentford (nyumbani)

-Oktoba 26 vs West Ham (ugenini)

-Novemba 2 vs Chelsea (ugenini)

Chanzo: Mwanaspoti