Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Antonio yamemkuta hadi kachukia soka

Skysports Michail Antonio West Ham 5239490 Staa wa Ligi Kuu England, Michail Antonio

Sat, 18 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Staa wa Ligi Kuu England, Michail Antonio amefunguka na kufichua kwamba alipatwa na tatizo la akili, ambalo lilimfanya atamani kuumia ili tu asicheze mpira.

Fowadi huyo wa West Ham United aliandamwa na tatizo hilo la akili kwa lililosababishwa na mambo ya ndani na nje ya uwanja kitu kilichomfanya achukue soka.

Antonio, 34, anafichua, wakati anajitafuta awe mchezaji bora zaidi uwanjani, alipigwa na kitu kizito baada ya mkewe kutaka talaka, kitu kilichomwaathiri kwa kiwango kikubwa na kulazimika mtu wa saikolojia kumweka sawa kurudi kwenye mstari.

Staa huyo wa kimataifa wa Jamaica, Antonio alikumbushia tukio la Desemba 2022 ambalo lilimweka kwenye mazingira ya kuchukua mpira, akisema: “Nilianza kuchukua mpira.”

“Na nilianza kujichukia, sifurahii mpira,” alisema na kuongeza: “Wakati wa mechi, ilikuwa najisemea ‘sifurahii soka kabisa’. Nilikuwa hovyo sana.

“Sikufunga bao kuanzia Desemba hadi nadhani ilikuwa Machi au Aprili. Nilikuwa najiona nimeshuka. Na baada ya hapo nilikwenda Jamaica na kufurahia soka kwa sababu za ajabu kabisa. Lakini, ukweli nilikuwa naomba nipate majeraha. Ilikuwa, ‘nataka niumie, nataka nipande muda wa kupumzika.’ Baadaye nilijifikiria mwenyewe, ‘Nina miaka 33. Sipaswi kucheza kwa kiwango hiki, sitapewa mkataba mpya.’”

Dili la Antonio huko West Ham litafika mwishoni mwa msimu huu, licha ya kwamba kuna kipengele cha kuongeza miezi 12 kama pande zote mbili zitafikia makubaliano.

Fowadi huyo wa zamani wa Nottingham Forest na Sheffield Wednesday amefunga mabao saba katika mechi 31 alizocheza msimu huu, huku mabao matatu amefunga katika mechi tano za mwisho.

Chanzo: Mwanaspoti