Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anthony aweka rekodi hii Man United

Anthony Record United.jpeg Mchezaji wa Man United, Anthony

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Manchester United Antony Santos amefanikiwa kuweka rekodi kwa kufunga magoli matatu katika michezo yake mitatu ya kwanza ya ligi kuu ya Uingereza.

Antony anakua mchezaji wa kwanza wa Manchester United kufunga magoli matatu kwenye michezo mitatu ya kwanza ya ligi kuu England, Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye alisajiwa na klabu hiyo kutokea klabu ya Ajax kwa rekodi ya Usajili ya paundi milioni 100.

Antony alicheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Arsenal ambapo klabu ya Manchester United ilifanikiwa kupata ushindi wa goli tatu kwa moja huku goli la kwanza la mchezo huo likifungwa na mchezaji huyo.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Ajax Amsterdam alifanikiwa kufunga katika michezo yake miwili iliyofata katika ligi hiyo ambayo ilikua ni dhidi ya klabu ya Manchester City ambapo waliambulia kipigo cha magoli sita kwa matatu huku mchezaji huyo akifunga bao la kwanza kati ya matatu United waliyopata kwenye mchezo huo.antonyMchezaji huyo raia wa Brazil tangu atue klabuni hapo ameonekana kuendana na mazingira haraka klabuni hapo tofauti na wachezaji wengine ambao huwachukua mda kufanya vizuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live