Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anthony Martial kuwekwa Sokoni mwisho wa Msimu

Anthony Martial Train Anthony Martial

Sun, 5 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Ufaransa Anthony Martial inaelezwa klabu hiyo imepanga kumuuza katika dirisha kubwa majira ya joto.

Mshambuliaji Martial ambaye amejiunga na klabu ya Manchester United mwaka 2015 chini ya kocha Louis Van Gaal hajafanikiwa kuonesha ubora ambao mabosi wa klabu hiyo waliutarajia wakati wanamsajili kutokea As Monaco, hivyo chaguo lao kwasasa ni kumpiga bei mchezaji huyo.

Klabu ya Manchester United wanaelezwa kuhitaji kumuuza mshambuliaji huyo ili waweze kupata kiwango fulani cha pesa ili kuweza kuongezea kupata mshambuliaji mwingine ndani ya klabu hiyo ambaye atakuja kuonesha ubora mkubwa.

Majeraha yanaeleza kua sababu ya Manchester United kufikiria kuachana na Martial kwani mshambuliaji huyo amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara na kushindwa kuonesha ubora wake,Majeraha yamemfanya mchezaji huyo kua kwenye kipindi kigumu zaidi klabuni hapo.

Washambuliaji ambao wanaelezwa kuchukua nafasi ya Anthony Martial ndani ya klabu ya Manchester United ni pamoja na Victor Osimhen anayekipa ndani ya klabu ya Napoli na mshambuliaji wa kimaaifa wa Uingereza Harry Kane, Hao ndo washambuliaji ambao Man United inaona wana ubora wa kuitumikia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live