Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Angola ipewe maua yake

Ecd171539a31aa8685e013231429bbe6.jpeg Angola ipewe maua yake

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Staa wa Angola, Gelson Dala, juzi alifunga mabao mawili na kuipeleka nchi hiyo hatua ya robo fainali ya Michuano ya Afcon 2023, ambapo sasa itavaana na Nigeria ambayo iliichapa Cameroon mabao 2-0 kwenye mchezo mwingine.

Timu zote mbili zilimaliza mchezo huo zikiwa pungufu baada ya wachezaji wawili kupewa kadi nyekundu, kipa wa Angola Neblu alikuwa wa kwanza kupewa nyekundu katika dakika ya 17 tu ya mchezo. Angola wakiwa 10 uwanjani wakafunga kibabe bao la kuongoza kupitia kwa Delson.

Muda mchache baadaye, beki wa Namibia, Lubeni Haukongo, alifuata naye kwa kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na hivyo timu zote mbili zilicheza muda mwingi wa mchezo zikiwa pungufu.

Hii ni mara ya kwanza Angola inakwenda hatua ya robo fainali kuanzia mwaka 2010.

Sasa Angola itavaana na vigogo Nigeria kwenye hatua ya robo fainali, katika mchezo unaotajwa kuwa mkali kutokana na ubora ulioonyeshwa na timu zote na utachezwa Ijumaa hii.

Hii ni mara ya tatu Angola inafika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya Afcon ikiwa awali ilikuwa haipewi nafasi kubwa ya kufanya hivyo.

Chanzo: Mwanaspoti