Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Ange Postecoglou ametajwa kuwania tuzo ya kocha bora wa mwezi wa kumi ikiwa ni mara ya tatu mfululizo anawania tuzo hiyo baada ya kuchukua tuzo mbili zilizopita.
Kocha Ange Postecoglou alifanikiwa kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi mara mbili ambapo ni mwezi wa nane na mwezi wa tisa, Huku akitajwa tena kuwania tuzo ya mwezi wa kumi akichuana na makocha wengine watatu.
Kocha huyo wa zamani wa klabu Rangers ya Scotland ataungana na makocha wengine watatu ambao ni Mikel Arteta wa klabu ya Arsenal, Kocha Jurgen Klopp wa Liverpool, na kocha wa klabu ya Aston Villa Unai Emery.
Kocha huyo wa klabu ya Tottenham amekua na msimu mzuri sana kwenye ligi kuu ya Uingereza na mpaka sasa hajafanikiwa kufungwa mchezo hata mmoja ambapo mpaka sasa klabu yake inaongoza kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.
Ange Postecoglou ndani ya mwezi wa kumi amefanikiwa kushinda michezo yote mitatu ambayo klabu yake imecheza, Huku makocha wote watatu waliobaki ambao anashindana nao kwenye tuzo hawajafanikiwa kushinda michezo mitatu wote wamechukua alama saba tu hivo hii inaonesha kocha huyo ana nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya tatu mfululizo.