Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Andy Carroll anaswa na mchepuko siku chache kabla ya ndoa

Andy Caroll Anndy Caroll na mchepuko

Sun, 5 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

STRAIKA Muingereza, Andy Carroll, amepigwa picha akiwa chumbani kitandani kimahaba na mrembo mmoja, zikiwa zimebaki wiki mbili tu kabla ya ndoa yake na mtangazaji, Billi Mucklow.

 

Carroll, 33, katika picha hizo, anaonekana akiwa amechoka taabani akiwa amelala pembeni ya mrembo Taylor Jane Wilkey.

 

Picha zake hizo zimesambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii huku rafiki wake wa karibu akinukuliwa akisema: “Hii ni mbaya sana huku ndoa ikiwa karibu kabisa.”

Lakini mrembo Taylor amejitetea akisema: “Sikulala naye, haikuwa hivyo, tulikuwa watatu kitandani. Ilikuwa ni siku nzima hadi usiku tukinywa, tangu saa sita (mchana), ilikuwa ni siku ya pombe. Andy alikuwa hajiwezi, wote tulikuwa tumelewa. Hakuna ngono yoyote iliyotokea.”

 

Carroll ambaye mara ya mwisho ameichezea West Brom kuanzia Januari, 2022 hadi mwisho wa msimu huu, amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: