Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Andrew Robertson Kukosa Mchezo Dhidi ya Chelsea

Andy Robertson Andrew Robertson

Sat, 25 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinzi wa kushoto wa klabu ya Liverpool Andrew Robertson ataukosa mchezo wa tarehe 2 January wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Chelsea baada ya mchezo wao wa Boxing day dhidi ya Leeds kuahirishwa.

Robertson anaitumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu kufuatiwa kuonyeshewa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwenye mchezo dhidi ya Tottenham wikiendi iliyopita, pia atakosa mchezo wa Carabao Cup dhidi ya Leicester.

Kukosekana kwake nafasi yake itachukuliwa na Kostas Tsimikas ndiyo atakeyeziba pengo lake, Tsimikas amecheza michezo 13 tu msimu huu mpaka sasa ikijumuisha michezo mitatu aliyoanza, pia lionyesha kiwango cha kuvutia alipochukua nafasi ya Robertson pale alipokuwa majeruhi.

Ingawa mchezo dhidi ya Leeds umahairisha mpaka hapo tarehe itakapopangwa tena kutokana na mlipuko wa Uviko-19 lakini bado Andrew Robertson hatakuwepo kwenye safari ambayo majogoo watasafiri kwenda darajani kutafuta pointi tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live