Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Andrew Arshavin: Jasusi wa Urusi aliyejificha kwenye soka

AndreyArshavin 2890501 Andrew Arshavin

Tue, 10 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unamkumbuka Andrey Sergeyevich Arshavin? Wengi wanamkumbuka Andrey Arshavin, kama winga machachari aliyekiwasha ndani ya klabu ya Arsenal.

Lakini duru za kijasusi ulimwenguni zinamtambua kama jasusi kutoka katika Shirika la Ujasusi la Urusi, Federal Security Service (FSB) akitekeleza "mission" ngumu ya kuipeleleza serikali ya Uingereza.

Ilikuwaje?!

Mnamo mwaka 2012, kuna nyaraka zilivuja kwenye jengo moja lililopo mitaa ya Fort Meade, huko Maryland nchini Marekani, ambapo jasusi mmoja kutoka katika Shirika la Kijasusi la National Security Agency (NSA) nchini Marekani, aliijulisha serikali ya Uingereza akifichua siri ya kwamba mchezaji wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Urusi, Andrey Arshavin, alikuwa jasusi wa Urusi aliyekuwa na jukumu ya kuipeleleza serikali ya nchi hiyo, akijivalisha uhusika wa Mwanasoka machachari.

Andrey Arshavin, akitambuliwa kwa jina la ‘Red Fox’, aliandaliwa na Kremlin, katika mpango maalumu wa kijasusi, mhusika akiwa Bwana Sergei Rachmaninoff, ambaye anatambulika kama "The Brainchild of Kremlin Chief", kwani ndiye aliyefadhili mafunzo ya Arshavin akiwa kama wakala wake na akashiriki kwa kiasi kikubwa kuhakikisha mchezaji huyo anasajiliwa kwenye ya klabu ya Zenit St. Petersburg ya nchini Urusi ikiwa ni hatua za awali za safari yake ya nchini Uingereza.

Kwa mujibu wa Digital Spy Forum, wanaeleza kuwa, Arshavin alipenyezwa kwenye klabu ya Zenith St. Petersburg akiwa kama mwanasoka ambapo lengo kuu lilikuwa kuhakikisha anasajiliwa kwenye moja ya vilabu vikubwa vinayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza (English Premier League).

Kabla ya kuanza "mission" yake, Arshavin alipewa jina maalumu (Code Name) akiitwa Red Fox. Akiwa Zenith St. Petersburg zikaibuka tetesi kuwa mchezaji huyo anahitajika na klabu ya Barcelona ya nchini Spain, dili hilo likamsukuma kocha wa Arsenal wakati huo, Profesa Arsene Winger kuingilia kati na kumsajili mchezaji huyo. January 31, 2009 alitangazwa rasmi kujiunga na klabu ya Arsenal maarufu kama The Gunners.

Adrew Arshavin alisakata soka ndani ya klabu ya Arsenal katika awamu mbili. Awamu ya kwanza, kuanzia 2009 hadi 2012, kisha achukuliwa kwa mkopo na klabu yake ya zamani ya Zenith St. Petersburg. May 31, 2012, akarejea tena Arsenal na msimu uliofuata akaondoka rasmi klabuni hapo na kutimkia Zenith St. Petersburg. Inaelezwa kuwa, hii ni baada ya kukamilisha "mission" yake.

Baada ya kuvuja kwa taarifa hii, inaelezwa kwamba hata taarifa za mchezaji huyo kutakiwa na klabu ya Barcelona hazikuwa na ukweli wowote, bali zilitengenezwa tu kama tetesi ili kumpa thamani mchezaji huyo na kuvivutia vilabu vikubwa vya nchini Uingereza.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, Warusi wenzake, Roman Pavlyuchenko na Pavel Pogrebnyak, ni majasusi wenzake wa Kremlin, nao walitumwa nchini Uingereza kwa majukumu ya kusaidia ujasusi wa Arshavin, na baadaye kumsaidia katika kutoroka kwake.

Hivi karibuni, Shirika la Ujasusi la Uingereza limefanya mawasiliano na Huduma ya Siri ya Ufaransa wakijaribu kuchunguza kama kocha Arsene Wenger wa Arsenal, alikuwa sehemu ya njama za Warusi.

NB: Makala hii itasikika kwenye DRIVE SHOW ya East Africa Radio, kuanzia saa 12: 35 jioni. Tafadhali usikose kusikiliza.

Imeandikwa na;- Hilal Kanal Dar es Salaam, Tanzania Sept 10, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live