Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa la Colombia, Andres Escobar Saldarriaga alikua anacheza kama beki wa timu ya taifa, lakini pia aliichezea Atletico Nacional, BSC Young Boys nickname aliiitwa ‘The Gentlemen’.
Mnamo Juni 22, 1994 kwenye michuano ya Kombe la Dunia ‘FIFA World Cup’ utakumbuka goli la kujifunga la mchezaji huyu katika mechi ya Colombia dhidi ya USA iliosababisha kushindwa kuendelea na michuano.
Andrés Escobar, ambaye alikuwa kapteni wa timu ya Taifa ya Colombia, aliheshimika na kupendwa na kila mtu, alifahamika kwa ukimya wake, nidhamu na umahiri katika majukumu yake, alijifunga wakati Colombia ilipopoteza mchezo huo dhidi ya Marekani kwa bao 2-1 na kuondolewa katika mashindano hayo.
Baada ya michuano Escobar aliamua kurudi Colombia badala ya kwenda Las Vegas kwa ndugu zake ikiwa ni siku tano tu baada ya kutolewa katika michuano ya World Cup.
Siku 10 baadaye, Julai 2, 1994, asubuhi, Andrés Escobar, jamaa alipofika aliwaita rafiki zake katika klabu ya pombe, alivamiwa na kundi la vijana wakiwa na silaha nje ya klabu ya starehe iliyipo jirani na nyumbani kwao, Medellín, mji wa pili kwa ukubwa COlombia na maarufu kwa biashara ya dawa.
Vijana hao walionekana wakibishana wawili kati ya wale vijana walichukua bastola na kumpiga risasi. Wauwaji walikua kila wakimpiga risasi moja wanatamka neno GOOAAL! Walimpiga Risasi sita wakimuacha damu zikimvuja na kupoteza maisha.
Vijana hao walisema bao alilojifunga Escobar na kuwapa ushindi Marekani limewanyima mamilioni ya pesa vijana hao ambao walikuwa wamebet.
Usiku wa kesho yake, polisi walimkamata kijana waliyeamini ndiye alihusika na mauaji hayo. Kijana Humberto Castro Muñoz alikuwa bodigadi na dereva wa kundi la Gallon brothers, vijana waliokuwa maarufu kwa uhalifu hasa wa biashara za dawa za kulevya.