Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Andre Onana arudisha maneno kwa mashabiki

Onana Vs Wolves Foul Andre Onana arudisha maneno kwa mashabiki

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: Dar24

Mlinda Lango wa Manchester United, Andre Onana amesema alikuwa anajimini kwamba Penati isingetolewa baada ya kugongana na Mshambuliaji wa Wolves, Sasa Kalajdzic katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu England iliyochezwa Jumatatu (Agosti 14).

Timu ya Erik ten Hag iliponea chupuchupu kulimwa Penati dakika za majeruhi kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi Wolves katika Uwanja wa Old Trafford.

Hata hivyo, Kocha wa Wolves, Gary O’Neil alikuja juu baada ya Mwamuzi kutotoa Penati kwani aliamini Mshambuliaji wake, Kalajdzic aliangushwa eneo la hatari na kipa huyo Mcameroon aliyesajiliwa kwa Pauni 47 Milioni kutoka Inter Milan.

VAR ilirudia picha tukio zima lakini refa aliyechesha mchezo huo, Simon Hooper akaruhusu mpira uendelee na kumlima kadi ya njano kocha wa Wolves kutokana na kupinga maamuzi yake.

Kufuatia tukio hilo Onana alisisitiza hakuamini kama refa angeruhusu penalti kupigwa baada ya kugonga na straika wa Wolves.

“Kama kipa unatakiwa kufanya uamuzi, wakati mwingine unakuwa sawa na uamuzi yako, wakati mwingine unakosea, nilifanya maamuzi na nimewajibika kwa kila kitu,” alisema

Baadhi ya mashabiki walitoa maoni kuhusu kauli ya Onana kupitia mitandao ya kijamii na mmoja akaandika: “Namkubali sana Onana kutokana na kujiamini kwake.” Mwingine akaandika “Kama unamchukia Onana basi msimu utakuwa mrefu sana.” Mwingine akadai kutokana na tabasamu lake anafahamu kwamba alifanya makosa.

Chanzo: Dar24