Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Andambwile aomba radhi Mbeya City kisa Singida BS

Mbeya Vs Singida Big Radhi Andambwile aomba radhi Mbeya City kisa Singida BS

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mbeya City na Singida Big Stars zimeshindwa kutambiana baada ya kutoshana nguvu ya bao 1-1 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Sokoine jijini hapa.

Sare hiyo imekuwa na faida zaidi kwa Singida kutokana na kukusanya pointi nne dhidi ya wapinzani hao kwani mchezo wa mzunguko wa kwanza wakicheza nyumbani walishinda mabao 2-1.

Zifuatazo ni dondoo za mchezo huo

Azizi Andambwile anafunga bao lake la kwanza msimu huu lakini akiwafunga waajiri wake wa zamani na kumfanya kushindwa kushangilia akionesha ishara ya kuwaomba radhi.

Juma Shenvuni anakuwa beki wa tisa kufunga bao Ligi Kuu akiungana na Djuma Shaban, Kibwana Shomari na Yanick Bangala (Yanga), Jumanne Elfadhir (Prisons), Mohamed Hussein na Henock Inonga (Simba) Denis Bukenya (Kagera Sugar) na Hassan Mohamoud wa Mbeya City.

Nickson Kibabage kutoka Mtibwa Sugar inakuwa mechi yake ya kwanza kuitumikia Singida Big Stars tangu aungane nao katika dirisha hili dogo akitokea benchi kuchukua nafasi ya Deus Kaseke.

Mchezaji wa Mbeya City Brown Mwankemwa alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na nafasi yake kujazwa na Jukumu Kibanda.

Mbeya City inafikisha mechi saba mfululizo nyumbani kwenye uwanja wa Sokoine bila kupata pointi tatu kati ya michezo 11 iliyocheza uwanjani hapo na kufikisha pointi 21 nafasi ya nane.

Singida Big Stars inajihakikishia pointi nne kwenye uwanja huo baada ya awali kuwalima Tanzania Prisons mabao 2-1 na leo inaondoka na pointi moja na kufikisha 31 baada ya mechi 17 ilizocheza.

Kocha mkuu wa Singida Big Stars, Hans Paluijm amesema walikuwa na uwezekano wa kushinda mechi hiyo lakini nafasi walizopata walishindwa kuzitumia mastraika wake.

"Hata hali ya uwanja ilikuwa tofauti na mchezo uliopita lakini tunashukuru kwa pointi nne tulizopata ugenini japokuwa tulihitaji alama sita," amesema Pluijm.

Kocha msaidizi wa Mbeya City, Anthony Mwamlima amesema baada ya mechi iliyopita kupoteza 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji leo wanashukuru kwa pointi moja huku akikiri kuwa bado benchi la ufundi halijaridhishwa na kiwango cha nyota wake.

"Hii ni ligi sisi tunaandaa timu kwa lengo la kushinda lakini matokeo ndio hivyo hawa nao ni binadamu makosa tunaenda kuyafanyia kazi kwa ajili ya mchezo ujao" amesema Mwamlima.

Chanzo: Mwanaspoti