Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ancelotti hana mpango na straika Januari

Vinicius Jr Ancelotti .png Ancelotti hana mpango na straika Januari

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amezungumzia mipango yake katika usajili wa dirisha dogo mwezi Januari.

Madrid, ambayo sasa inaongoza katika mbio za ubingwa wa La Liga ikiwa kileleni baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Granada, haitafanya usajili wa straika katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari, Ancelotti amethibitisha.

Akizungumza na waandishi wa habari alipoulizwa kuhusu usajili wa mwezi Januari, Muitaliano huyo alisema: “Mshambuliaji mpya Januari? Hapana. Timu itabaki na wachezaji walewale hakuna mabadiliko yatakayofanyika, kila kitu kitakuwa sawa.”

Los Blancos ilifanya usajili wa wachezaji watano katika usajili uliopita, ikiwa ni pamoja na uhamisho wa kiwango cha juu wa Jude Bellingham kutoka Borussia Dortmund.

Pia walimnunua Joselu kwa mkopo kutoka Espanyol kuchukua nafasi ya Karim Benzema, ambaye aliondoka baada ya mkataba wake kumalizika na kujiunga na Al-Ittihad ya Ligi Kuu Saudi Arabia.

Ancelotti anatumia mfumo mpya wa 4-4-2 huku Rodrygo na Vinicius Junior wakicheza mbele na Bellingham akicheza nyuma kidogo ya washambuliaji hao wawili.

Mabadiliko ya mbinu yamefanya kazi kwa Madrid hadi sasa kwani imefunga mabao 44 katika mashindano yote.

Bellingham ndiye mfungaji bora wa Madrid kwa sasa akiwa amefunga mabao 15 akifuatiwa na Rodrygo aliyefunga mabao manane.

Kutokana na takwimu nzuri katika safu ya ushambuliaji, kocha huyo mwenye umri wa miaka 64, anaamini kikosi chake kitafanya vizuri licha ya Vinicius Jr kuwa nje ya dimba hadi mwezi Februari mwakani.

Chanzo: Mwanaspoti