Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ancelotti bado yupo sana Madrid

Ancelotti Akanusha Kuelekea Timu Ya Taifa Ya Brazil Carlo Ancelotti.

Sat, 30 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Carlo Ancelotti amesaini mkataba mpya na Real Madrid licha ya kuhusishwa na timu ya taifa ya Brazil mkataba wake utakapomalizika mwakani.

Taarifa ziliripoti Ancelotti alitarajiwa kuwa kocha wa Brazil kwa ajili ya michuano ya Copa America itakayoanza mwakani, hata hivyo ameongeza mkataba utakaomweka Madrid hadi mwaka 2026.

Madrid imetoa taarifa rasmi kupitia tovuti yao; "Real Madrid na Carlo Ancelotti tumekubaliana kusaini mkataba mpya hadi 2026. Katika miaka mitano akiwa kama kocha, ameshinda mataji 10, makombe mawili ya Ligi Mabingwa Ulaya, La Liga moja, Copa del Rey mawili, Super Cup moja,"

"Carlo Ancelotti ndiye kocha pekee aliyeshinda mataji manne ya Ulaya katika historia ya mashindano hayo, pia ameshinda mechi nyingi za michuano ya ulaya (118). Pia ameshinda mataji matano makubwa Ulaya (England, Hispania, Ufaransa na Ujerumani),"

Tetesi za Ancelotti kuhusu hatima yake imechukua muda wa miezi miwili, huku akitajwa kuwa atakuwa mrithi wa kocha wa Brazil, Tite baada ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana.

Licha ya Madrid kushindwa kubeba La Liga na Ligi Mabingwa Ulaya, Ancelotti ameaminiwa na mabosi kutokana na utendaji wake wa kazi.

Makocha kama Roberto De Zerbi (Brighton) na Xabin Alonso (Bayer Leverkusen) walihusishwa na Madrid, hata hivyo tetesi za hatima yake zimefikia tamati.

Kocha huyo atarejea kukiongoza kikosi chake kwenye mechi ya La Liga dhidi ya Mallorca, itakayochezwa Januari 3 kabla ya mechi ya Copa del Rey siku tatu baadaye, halafu itamenyana na Atletico Madrid January 10 katika michuano ya Supercopa de Espana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live