Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ancelotti: Vinicius Jr anatendewa sivyo

Carlo With Vinicious Ancelotti: Vinicius Jr anatendewa sivyo

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, amesena Vinicius Junior anatendewa vibaya zaidi uwanjani kuliko mchezaji yeyote ambaye amemfundisha katika maisha yake ya soka.

Vinicius alifunga bao pekee la Madrid katika sare ya 1-1 ya raundi ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya RB Leipzig kwenye Uwanja wa Bernabeu Jumatano, lakini pia alibahatika kutopata kadi ya njano kwa kumsukuma nahodha wa Leipzig, Willi Orban.

Wikiendi iliyopita, fowadi huyo wa Brazil alipigiwa filimbi mara kwa mara na umati wa watu huko Mestalla wakati Madrid ilipotoka sare ya mabao 2-2 na Valencia mchezo ambao pia alifunga mara mbili baada ya kubaguliwa na kundi la mashabiki kwenye mechi hiyo hiyo msimu uliopita.

“Nimeangalia nyuma kidogo, katika historia, takwimu, na sijawahi kuona kama Vinicius,” alisema Ancelotti katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mchezo wa wa La Liga wa Madrid dhidi ya Celta Vigo.

“Anapigwa teke, anapigiwa filimbi, anatukanwa. Na anafanya nini? Anafunga mabao na kutoa pasi za mabao. Halafu natakiwa kuzungumza naye kuhusu mtazamno wake? Hapana!

“Kila mtu anapaswa kubadili mtazamo wake kuhusu Vinicius. Katika historia yangu binafsi, mchezaji mwenye kipaji kikubwa hajawahi kuteseka na mambo ambayo Vinicius anayo. Huko Vallecas (dhidi ya Rayo Vallecano) alikatwa karate kichwani, na hakukuwa na hata kadi ya njano. Sasa kila mmoja anaomba kadi nyekundu kwa kusukuma dhidi ya Leipzig.”

Vinicius amefunga mabao tisa katika mechi 18 za La Liga msimu huu, na matatu katika mechi tano za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika kikosi cha Madrid, amezidiwa tu na Jude Bellingham, ambaye alikosa mechi ya Celta baada ya kufungiwa michezo miwili kwa kutolewa nje kwenye sare ya Valencia.

Bellingham alitolewa nje baada ya filimbi ya mwisho kwa kupinga uamuzi wa mwamuzi kumaliza mchezo sekunde chache kabla ya kupiga mpira wavuni kwa kichwa, kwa kile ambacho kingekuwa bao la ushindi.

“Tulikata rufaa kwa sababu tulifikiri adhabu ilikuwa kubwa,” Ancelotti alisema.

“Hakukuwa na matusi ripoti ya mwamuzi ilisema hivyo Kamati ya nidhamu ya RFEF ilitathmini njia ya fujo ambayo alienda kwa mwamuzi.

“Natumai hawana namba yake Bellingham wakati mwingine hulalamika kama kila mtu, lakini wachezaji wengi hufanya hivyo kwa njia ya kutia chumvi kuliko Bellingham. Bado tunafikiri adhabu hiyo sahihi.”

Chanzo: Mwanaspoti