Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ancelotti: Ubaguzi Dhidi ya Vinicius Jr Hauvumiliki

Vinicius Ancelotti Ancelotti na Vinicious

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vitendo vya kibaguzi dhidi ya winga wa kimataifa wa Brazil Vinicius Jr. havikubaliki na havipaswi kuvumilika, ni maneno ambayo kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti ameyasema kuelekea mchezo wa Kombe la Dunia ngazi ya klabu watakaocheza na Al Ahly.

Winga huyo amekuwa akikumbana na vitendo vya kibaguzi mara kadhaa na mara ya mwisho amezomewa na mashabiki wa Real Mallorca kwenye mechi ya Ligi Kuu iliyomalizika kwa Real Madrid kufungwa bao 1-0.

“Vinicius ni mhanga wa ubaguzi kitu ambacho mimi huwa sielewi msingi wake”, alisema Ancelotti.

Real watakutana na miamba ya soka ya Misri Al Ahly Jumatano hatua ya nusu fainali mtanange utakaopigwa Rabat, Morocco.

Mwezi Septemba alifanyiwa ubaguzi na mashabiki wa Atletico Madrid, Disemba mwaka uliopita pia alifanyiwa ubaguzi na mashabiki wa Real Valladolid kwenye ushindi wa Real wa bao 2-0.

Vinicius alizitaka mamlaka zinazohusika kushughulikia matatizo hayo kwa uangalifu huku akisisitiza kuwa kumfanyia ubaguzi hakuwezi kumfanya aache kufurahia maisha ya kandanda ikiwemo kucheza akifunga goli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live