Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ancelotti: Tutapambana na Barcelona kutetea Ubingwa

Carlo Ancelotti.jpeg Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti

Wed, 15 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amesisitiza kua mabingwa hao watetezi wa kombe la La Liga watapambana na vinara wa ligi hiyo kwasasa kuhakikisha wanatetea taji hilo tena msimu huu.

Kocha Ancelotti anasema kua klabu ya Real Madrid bado ipo kwenye mbio za kuwania taji hilo licha ya kua nyuma kwa alama 11 dhidi ya vinara klabu ya Barcelona, Ambapo klabu ya Real Madrid ipo nyuma kwa mchezo mmoja ambao itacheza na Elche siku ya jumatano.

Klabu ya Real Madrid imekua haina muendelezo mzuri katika ligi kuu ya Hispania baada ya kushinda michezo minne pekee kati ya tisa iliyopita ya ligi hiyo msimu huu, Huku wakipoteza michezo mitatu na kusuluhu michezo miwili jambo ambalo linatoa ushara mbaya kwa klabu hiyo kua huenda wakashindwa kutetea taji hilo.

Kocha Carlo Ancelotti wakati anazungumza na wanahabari kulekea mchezo wa kesho dhidi ya Elche na kusema kwamba “Wazo nililo nalo ni kushinda kwakua ukishinda unataka kurudia kushinda,Kurudia kushinda ni motisha kwetu, Tuna changamoto kwenye La liga lakini tutakwenda kupambana”

Kocha Carlo Ancelotti amesema kua ataendela kuwakosa baadhi ya nyota wake katika kikosi cha Real Madrid kama Thibaut Courtois ambaye hakuwepo hata kwenye michuano ya klabu bingwa ya dunia, Lakini pia kiungo Toni Kroos ambaye nae atakosekana kesho, Lakini akieleza wachezaji wote hao watakuepo dhidi ya Osasuna siku ya jumamosi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live