Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ancelotti: Matokeo ya Ballon d’Or yaheshimiwe

Anceloti Meneja wa Real Madrid, Carlo Anceloti

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Real Madrid Carlo Ancelotti alikuwa na mkutano na wandishi wa habari siku ya Jumanne kuelekea mchezo wa Real Madrid dhidi ya Athletic Bilbao katika LaLiga.

Waandishi hawakuuliza maswali kuhusu mchezo huo pekee pia waligusia kuhusu tuzo za Ballon d’Or zilizofanyika siku ya Jumatatu usiku.

Ushindi wa Leo Messi umezua mjadala mkubwa, lakini Ancelotti anahisi kwamba matokeo lazima yapewe heshima, ingawa alitamani mshindi wa Real Madrid katika toleo la mwaka ujao.

“Lazima uheshimu matokeo ya Ballon d’Or 2021. Messi ameshinda na bado ni mchezaji mzuri. Na hakuna cha kuongeza,” alisema.

“Kwa wachezaji, tuzo za mtu binafsi ni muhimu, lakini ikiwa hawatashinda, sio suala.

“Natumai mwaka ujao, mchezaji wa Real Madrid atashinda. Benzema alikuwa na msimu mzuri na alimaliza wa nne. Ataendelea na motisha ya kujaribu kuwa wa kwanza.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live