Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ancelotti, Guardiola wafikiriwa Brazil

Pep And Ancelotti 1140x630 Ancelotti, Guardiola wafikiriwa Brazil

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: dar24.com

Shirikisho la Soka nchini Brazil ‘CBF’ linafikiria kumuajiri Kocha Mkuu Mpya wa Timu ya Taifa hilo, baada ya Kocha Tite kutangaza kustaafu siku chache baada ya kushindwa kuivusha ‘O Canarinho’ katika hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia iliyomalizika nchini Qatar mwishoni mwa juma lililopita.

Brazil iliondoshwa na Craotia katika Hatua ya Robo Fainali kwa changamoto ya Mikwaju ya Penati, na kufuta kabisa ndoto za taifa hilo kurejesha heshima ya kuwa Mabingwa wa Dunia iliyopotea tangu mwaka 2022.

Tayari ‘CBF’ inahusishwa na mpango wa kumuajiri Kocha kutoka nje ya Brazil, huku Majina ya Makocha nguli Barani Ulaya Pep Guardiola wa Manchester City na Carlo Ancelotti wa Real Madrid yakitajwa kila kukicha.

Hata hivyo Ancelotti anapewa kipaumbele cha kuchukua nafasi hiyo, huku Taarifa zikieleza kuwa angekuwa huru kwa sasa angefanikisha mpango wa kukabidhiwa jukumu la kukiongoza kikosi cha Brazil, lakini Mkataba uliopo kati yake na Real Madrid unaonekana kuwa kikwazo.

Hata hivyo, alipoulizwa kwenye kituo cha Redio cha Italia Radio1, Ancelotti alijibu kwamba ana furaha katika mji mkuu wa Hispania, Madrid.

“Kufundisha Brazil? Sijui nini kitatokea katika siku zijazo, ninaishi wakati huu. Mimi ni mkubwa na ninajisikia vizuri Madrid, bado tuna malengo mengi ya kufikia,” alisema Ancelotti.

“Kuna wakati wa kufikiria juu ya siku zijazo. Nina mkataba unaoisha 2024 na ikiwa Real Madrid hawataniondoa, sitahama.”

Ancelotti aliacha mlango wazi endapo atapenda kubadili mwelekeo katika siku zijazo, lakini anaonekana kutaka kuona mkataba unaendelea pale Madrid.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 63 hapo awali alisema kuwa hii itakuwa kazi yake ya mwisho na anakusudia kustaafu baada ya kuondoka Real Madrid.

Chanzo: dar24.com