Kocha Mkuu wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amewapa onyo wachezaji wake kwa kuwambia kuwa licha ya kupata ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘Uefa’ lakini bado wana kazi kubwa ya kufanya mbele ya wapinzani wao hao.
Kocha huyo ametoa kauli hiyo wakati leo Jumatano, Madrid watakuwa wenyeji wa Liver kwenye mechi ya marudiano ambayo itapigwa Uwanja wa Santioago Bernabeu. Madrid wataingia kwenye mechi hiyo wakiwa na kumbukumbu ya kushinda kwenye mechi ya kwanza nchini England kwa mabao 5-2.
Ancelotti amesema: “Tuna uzoefu wa mwaka jana dhidi ya Chelsea. Tuna mtaji wa mabao matatu, ndiyo maana tunapewa nafasi kubwa lakini kitu cha muhimu kuna dakika 90 za kucheza.
“Tunatakiwa kucheza kwenye ari ileile ya mechi ya kwanza. Tuna faida, lakini hatufikirii kwamba tunaweza kumiliki mchezo huu na matokeo ambayo tunayo, tunatakiwa kucheza dakika 90 tukiwa juu.”