Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amza wa Ihefu awazia mabao saba

Amza Mkuuu Amza wa Ihefu awazia mabao saba

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Ihefu FC, Moubarack Amza anatambua ana kazi nzito ya kuhakikisha anafunga zaidi ya mabao saba aliyomaliza nayo msimu uliyopita, akiwa na Coastal Union ya Tanga.

Tayari amefungua akaunti ya bao moja, akifunga dhidi ya Kagera Sugar,licha ya kukiri ugumu wa mechi za msimu huu, hazijamkatisha tamaa kuona hawezi kuingia kwenye ushindani wa kufunga mabao mengi.

“Ninachokiangalia ni nafasi, najitambua nimekuja Tanzania kufanya kazi, hivyo nitapambana kwa kadri niwezavyo, kutimiza malengo yangu,” alisema na kuongeza;

“Ligi ya Tanzania ina ushindani na kila msimu ushindani unaongezeka, lakini hiyo ni nzuri kwetu wachezaji inatufanya tuongeze bidii kujiweka fiti zaidi.”

Mchezaji mwingine wa timu hiyo, Rashid Juma alisema wanajipanga kuipambania timu yao, kuona msimu huu hawafanyi kazi ya kujikwamua kushuka.

“Ligi ilivyo ngumu, haitakiwi kulaza damu, tunatakiwa kuanza kupambana mwanzo mwisho,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live