Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amunike apigwa chini Timu ya Taifa ya Nigeria

Finidi Amunike.jpeg Amunike apigwa chini Timu ya Taifa ya Nigeria

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la soka la Nigeria limemteua mchezaji wa zamani wa Super Eagles Finidi George kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya Taifa ya Wanaume.

Finidi George, alikuwa amehudumu kwa miezi 20 kama Kocha Msaidizi wa José Santos Peseiro ambaye muda wake ulimalizika kama kocha mkuu wa timu hiyo.

Katika kipindi chake cha muda, George alisimamia mechi mbili za kirafiki nchini Morocco mwezi uliopita, ambapo timu hiyo ilimaliza mfululizo wa miaka 18 bila ushindi dhidi ya Ghana kwa ushindi wa 2-1 kabla ya kupoteza 0-2 dhidi ya Mali.

Jukumu la kocha huyo mpya wa Super Eagles litakuwa kuiongoza timu kupata ushindi katika mechi mbili muhimu za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Afrika Kusini na Jamhuri ya Benin mjini humo na Abidjan, ndani ya wiki chache zijazo.

Kocha George Finidi anachukua nafasi ya Amunike aliyetemwa hata kabla ya kuanza kazi ndani ya timu ya taifa ya Nigeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live