Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amuneke atimuliwa ukocha Misri baada ya mwezi mmoja

97669 Puic+amunike Amuneke atimuliwa ukocha Misri baada ya mwezi mmoja

Mon, 2 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Cairo, Misri. Kocha Emmanuel Amuneke ametimuliwa kuwa kocha wa Misr El-Makkasa ya Misri mwezi moja tangu alipopewa jukumu hilo sasa atakuwa mkurungezi wa akademi za klabu hiyo itakayofungua kituo cha kwanza hivi karibuni Tanzania.

El-Makkasa ilitangaza kumpa kazi ya ukocha Amuneke mwezi Februari 2 baada ya kuachana na kocha Ahmed Hossam Mido.

Klabu hiyo ilitoa taarifa yake jana Jumapili, kuwa kumtaja Ehab Galal kuwa kocha mpya anayechukua jukumu la Amuneke aliyepangiwa kazi nyingine.

"Tumefikia makubaliano na Ehab Galal kuiongoza timu kuanzia katika mchezo wa leo Jumatatu dhidi ya Aswan katika Ligi Kuu Misri," ilisema taarifa hiyo.

"Amuneke atakuwa mkurungezi wa akademi za klabu ambazo tumepanga kuzifungua katika sehemu mbalimbali barani Afrika, kituo cha kwanza kitafunguliwa hivi karibuni Tanzania", iliongeza taarifa ya El-Makkasa.

Amuneke aliiongoza El-Makkasa katika michezo mitatu tu dhidi ya Smouha na Al Entag Al Harbi akipata sare mbili za bao 1-1, kabla ya kufungwa 1-0 na Tala'ea El Gaish katika Kombe la Misri.

Pia Soma

Advertisement
El-Makkasa inapambana kujikwamua kushuka daraja ikiwa katika nafasi ya 16 na pointi 14.

Chanzo: mwananchi.co.tz