Kocha Mkuu, Adel Amrouche ametaja sababu ya kiungo mshambuliaji, Kelvin John anayecheza katika klabu ya Genk kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023; zinazotarajiwa kuchezwa Ivory Coast, ambapo amesema sababu kubwa ni makosa ya kinidhamu.
Kocha Mkuu, Adel Amrouche ametaja sababu ya kiungo mshambuliaji, Kelvin John anayecheza katika klabu ya Genk kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023; zinazotarajiwa kuchezwa Ivory Coast, ambapo amesema sababu kubwa ni makosa ya kinidhamu. Amrouche amefunguka hivyo muda mchache baada ya kutangaza kikosi cha timu ya Taifa kitakacho iwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo, ambapo katika mchujo wa kwanza, majina 31 yametajwa huku mchujo mwingine ukipangwa kufanyika baada ya mechi za kirafiki Cairo, nchini Misri.