Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amrouche ajipa matumaini Kombe la Dunia

Adel Amrouche Stars Amrouche ajipa matumaini Kombe la Dunia

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa timu ya taifa, ‘Taifa Stars’, Adel Amrouche amesema pamoja na kupoteza mchezo wao dhidi ya Morocco lakini nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 bado ni kubwa kwao.

Stars iliangukia pua Jumanne usiku ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam baada ya kufungwa mabao 2-0 na Morocco katika mchezo wa pili wa Kundi E.

Kocha huyo raia wa Algeria alikiri kuwa wapinzani wao walikuwa bora katika maeneo mengi jambo lililowapa wakati mgumu wachezaji wake ambao wengi wao wanakosa uzoefu.

“Nawapongeza wachezaji wangu walicheza kwa kujituma na kufuata maelekezo tuliyowapa, na hata mabao tuliyofungwa ni makosa ya mchezaji mmoja mmoja lakini pamoja na yote tulicheza na timu bora Afrika ambayo kupitia uzoefu wa wachezaji wao walifanya kila walichotaka, hongera kwao,” alisema Amrouche.

Kocha huyo alisema pamoja na kupoteza mchezo huo hawajakata tamaa kwani nafasi bado wanayo na mkakati wake ni kuendelea kuiandaa timu kwa kushirikiana na TFF ili kufanya vizuri mechi zijazo na hilo linawezekana kutokana na hamasa kubwa waliyonayo hivi sasa.

Kwa upande wa kocha mkuu wa Morocco, Walid Regragui alisema ulikuwa mchezo waliotarajia upinzani mkali kutoka kwa wenyeji wao kwa kuwa walikuwa nyumbani na walitoka kushinda ugenini dhidi ya Niger.

Alisema amefurahi kupata ushindi ambao umewaweka kileleni mwa msimamo wa kundi na malengo yao ni kushinda mechi zijazo ili kumaliza wa kwanza ingawa pamoja na ubora walionao hawatoidharau timu yoyote.

Kwa matokeo hayo, Morocco imekwea kileleni mwa kundi hilo kwa pointi tatu na mabao mawili wakifuatiwa na Zambia waliopo nafasi ya pili wakiwa na idadi kama hiyo ya pointi lakini wamefungwa mabao matatu.

Taifa Stars ni ya tatu ikiwa na idadi kama hiyo ya pointi sawa na Niger iliyopo nafasi ya nne na Congo Brazaville inashika nafasi ya nne ikiwa haina pointi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live