Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amroache aanza na mabadiliko haya dhidi ya Uganda

Msuva Himid Amroache aanza na mabadiliko haya dhidi ya Uganda

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Adel Amrouche ametoa kikosi chake cha kwanza kitakachoivaa Uganda kwenye mechi ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon 2023), mchezo utakaoanza saa 11:00 jioni katika uwanja qa Suez Canal, Musri huku kocha huyo akionekana kuanza na mabadiliko makubwa.

Amrouche ameanza na mabadiliko ya wachezaji na nafasi ambapo katika kikosi cha leo ameanza na mabeki wa kati asilia watatu, viungo asili wanne, washambuliaji wa kati wawili, winga mmoja, na kipa mmoja.

Aina hiyo ya wachezaji huenda ikabadili mfumo wa Stars uliozoeleka wa 4-4-2 na kuhamia 3-4-3 au 5-3-2 kutokana na uchezaji wa wachezaji hao katika mechi zilizopita katika klabu zao.

Katika eneo la ulinzi, Amrouche ameanza na kipa, Aishi Manula, mabeki Dickson Job, Novatus Dismas, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca.

Viungo ni Himid Mao, Mzamiru Yassin na Mudathiri Yahya huku Washambuliaji wakiwa Mbwana Samata na Said Khamis na winga Simon Msuva.

Kama Amrouche atachagua kucheza mfumo wa 3-4-3, huenda safu ya ulinzi ikaundwa na Job, Bacca na Mwamnyeto huku Novatus huku Novatus akisogea eneo la kiungo kuungana na Mao, Mudathiri na Mzamiru.

Eneo la mbele watakuwa Msuva, Samatta na Said.

Kama kocha atakuwa na mpango wa 5-3-2 basi msitari wa ulizi watakuwepo, Job, Novatus, Bacca na Mwamnyeto, kiungo watakuwa Mao, Mzamiru, Mudathir na mbele watakuwa Samatta na Said.

Lakini pia huenda mifumo hiyo ikawa inabadilika kutokana na aina ya uchezaji wa timu zote mbili.

Benchi wapo Beno Kakolanya, David Luhende, Kibwana Shomari, Ally Msengi, Feisal Salum, Kelvin John, Abdallah Mfuko, Sospeter Bajana, Edmund John, Yusuph Kagoma, Abdul Seleman na Ben Starkie.

Stars baada ya kupoteza mechi na Algeria ikichapwa 2-0 na kutoa sare ya bao 1-1 na Niger, inahitaji ushindi katika mechi ya leo dhidi ya Uganda na ile ya marudiano itakayopigwa Machi 18, mwaka huu Benjamin Mkapa ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu Afcon 2023 kutokea kundi lake F, lenye timu hizo nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live