Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amri Said aahidi makubwa Mwadui

6ac26569a7df35a4d2983d3acfbefe38 Amri Said aahidi makubwa Mwadui

Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BAADA ya kusaini mkataba wa miezi sita kukinoa kikosi cha Mwadui, Amri Said (pichani) ameahidi kurejesha ari ya upambanaji kwa wachezaji wa timu hiyo.

Uongozi wa Mwadui umeingia mkataba na Said baada ya kumtimua aliyekuwa kocha wake, Khalid Adam kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Akizungumza kutoka mkoani Shinyanga jana, Said alisema moja ya kazi waliyokubaliana ni kuhakikisha kikosi hicho kinafanya vizuri kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Tayari nimeshajiunga na Mwadui kwa mkataba wa miezi sita na kwa kipindi chote tumekubaliana kikosi kurejesha ushindani na kufanya vizuri michezo iliyosalia ya ligi,”alisema.

Alisema ameshaongea na viongozi wa timu hiyo kwa ajili ya kusajili wachezaji wapya wa kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kujipanga kwa michezo inayokuja.

“Nimeshaongea nao na wamekubali, kikubwa nasubiri waanze kazi ili nipate wachezaji kwa wakati niwaunganishe kwenye kikosi kabla dirisha dogo la usajili halijafungwa.”

Mwadui inashika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayoshirikisha jumla ya timu 18 ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza michezo 18 wakishinda minne, kupoteza 11 na kutoka sare mara tatu.

Chanzo: habarileo.co.tz