Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amri Kiemba afunguka alivyogombana na mganga

Amri Kiemba Amri Kiemba afunguka alivyogombana na mganga

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Amri Kiemba ameeleza kuwa kipindi anacheza mpira mambo ya uganga yalikuwa yanahusika kwenye klabu mbalimbali.

Kiemba ameeleza kuwa kipindi hicho alikuwa akiingia kwenye ugomvi na waganga kwa sababu alikuwa anaamini hawafanyi kazi na zaidi walitumia saikolojia tu ili timu zipate ushindi.

Katika kuthibitisha kuwa waganga walikuwa wanacheza na akili za wachezaji alikuwa akiwaomba waanze kuonyesha ujuzi wao mazoezini ndio waende kwenye mechi lakini walikuwa wanagoma kufanya hivyo.

“Mganga hawezi kuloga timu ambayo haina wachezaji wazuri ndio maana mkienda atawauliza timu mnayo?.

“Waganga siku zote huwa wanaangalia sehemu nne, golikipa ambaye huwa anamwambia mpira ukipigwa ruka utakufuata, namba tano, namba nane na mshambuliaji ambaye huwa anaambiwa akikaribia goli yeye alenge tu.

“Mimi nilikuwa na ugomvi na waganga, nilikuwa nawaambia waje waanzie mazoezini, waloge timu moja kati ya zile ambazo tutajigawa na walikuwa wanagoma.

“Mganga anacheza na saikolojia ya wachesaji tu, hata wewe unaweza kuwachanganya ukaamua kushika nyavu na kujifanya unazishona shona wakahisi unaloga,” amesema Amri Kiemba kupitia Clouds FM.

Matukio ya imani za kishirikina michezoni imekuwa ikiripotiwa mara kwa mara kwa kipindi cha hivi karibuni kwa wachezaji, timu na mashabiki wa timu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live