Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amrabat aitaka jumla Man United

Ten Hag With Amrabat Amrabat aitaka jumla Man United

Thu, 28 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Sofyan Amrabat amesema atakuwa mwenye furaha akifanikiwa kubaki Manchester United baada ya mkataba wake wa mkopo kufika tamati majira ya kiangazi mwakani.

Staa huyo wa kimataifa wa Morocco amejiunga Man United kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Fiorentina na Jumanne alionyesha kiwango bora katika mechi yake ya kwanza kuanzishwa uwanjani Old Trafford dhidi ya Crystal Palace kwenye Kombe la Ligi.

Amrabat, 27, alilazimisha uhamisho wa kutua Old Trafford kwa kipindi chote cha dirisha la majira ya kiangazi kabla ya kukamilisha dili hilo katika siku ya mwisho ya kufungwa usajili.

Na sasa ameelekeza nguvu zake kwenye kuisaidia Man United kushinda mataji msimu huu na amekuwa na matumaini makubwa ya kuwashawishi mabosi wa timu hiyo ili abaki jumla Old Trafford.

“Ningependa nibaki hapa, lakini sitaki kutazama sana mambo ya baadaye. Kwangu mimi kwa sasa ni mchezaji wa Manchester United. Kitu pekee nitafanya ni kujitolea kwa kila ninachoweza, nitajitahidi kusaidia timu," alisema Amrabat na kuongeza.

“Natumai tutakuwa na msimu mzuri, natumaini nitashinda kitu na baada ya hapo tutajua kitakachotokea.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live